Leo, tarehe 25 Machi 2025, Mhe. Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo, amekutana na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) inayoongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bw. Raymond Mndolwa, pamoja na Wahandisi wa Umwagiliaji kutoka mikoa mbalimbali, jijini Dodoma. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Dkt. Hussein Mohamed Omar, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula.

Katika kikao hicho, masuala ya kiutendaji yamejadiliwa, huku lengo kuu likiwa ni kukuza ushirikiano wa kazi kati ya Wizara ya Kilimo na wadau wengine, ili kuhakikisha malengo ya Serikali katika sekta ya kilimo yanatekelezwa kwa ufanisi, na hivyo kuimarisha huduma kwa wakulima wa Tanzania.
