Utiaji Saini wa Makubaliano ya Usimamizi wa Skimu za Umwagiliaji.

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imesaini makubaliano na Wakurugenzi wa Halmashauri 19 nchini kuhusu usimamizi na uendeshaji wa matunzo ya skimu za umwagiliaji kupitia Mradi wa Mifumo Himilivu ya Chakula (TFSRP).

Katika hafla hiyo, Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, ameitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) kushirikiana kwa karibu na Wakurugenzi wa Halmashauri katika utekelezaji wa miradi ya umwagiliaji nchini ili kuhakikisha miradi hiyo inakuwa endelevu na yenye tija kwa shughuli za kilimo.

Makubaliano haya yanahusu usimamizi wa skimu 23 zinazokarabatiwa kupitia mkopo wa masharti nafuu chini ya Mradi wa TFSRP. Katika utekelezaji wake, Tume imenunua magari 17 pamoja na mitambo ya uchimbaji wa visima 56,000, ambapo kisima kimoja kinalenga kumwagilia hekari 40 za mashamba ya wakulima.

Mradi wa TFSRP unagharimu jumla ya Dola za Marekani milioni 300, ambapo Tume ya Umwagiliaji imepata Dola milioni 70 kwa ajili ya:

✅ Uchimbaji wa visima 67,000
✅ Kuongeza eneo la umwagiliaji kufikia hekta 37,000
✅ Ununuzi wa mitambo 15 ya uchimbaji wa visima
✅ Ujenzi wa skimu mpya za umwagiliaji

Hafla hii imehudhuriwa na Wakurugenzi wa Halmashauri kutoka Morogoro Vijijini, Ifakara, Kongwa, Dodoma Jiji, Mufindi, Kilolo, Iringa Mji, Mbarari, Nzega, Korogwe, Lushoto, Moshi Mji, Meru, Sikonge, Igunga, Kilosa, Same, Hai, pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mwanga.

#KaziIendelee 🚜💧🌾 #Agenda1030

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *