Dodoma
11 Novemba 2025

Mapema leo katika Viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, nimewasili rasmi na kula kiapo cha uaminifu kabla ya uzinduzi wa Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Kumi na Tatu.

Katika tukio hili muhimu, nimeungana na wabunge wenzangu kutoka maeneo mbalimbali nchini kuanza majukumu ya kibunge ambayo yamelenga kulisimamia, kuliimarisha na kuliendeleza Taifa letu kwa manufaa ya Watanzania wote.

BASHE AVUNJA REKODI UZINDUZI WA KAMPENI NZEGA MJINI, WANANCHI WAJITOKEZA ATOA AHADI ZA MIAKA MITANO
BASHE AVUNJA REKODI UZINDUZI WA KAMPENI NZEGA MJINI, WANANCHI WAJITOKEZA ATOA AHADI ZA MIAKA MITANO

Napenda kutoa shukrani za dhati kwa wananchi wa Nzega Mjini kwa imani kubwa mliyonipa na kwa kunirudisha tena kuongoza jimbo letu kwa kipindi kingine cha miaka mitano chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan. Nawaahidi kuendelea kuwatumikia kwa uadilifu, bidii na uwazi, sambamba na kusukuma mbele ajenda za maendeleo tulizokubaliana wakati wa kampeni.

Vilevile, natoa shukrani kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuendelea kuniunga mkono na kunipa nafasi ya kulitumikia Taifa kupitia Bunge. Ninaahidi kuendelea kushirikiana kikamilifu na chama chetu katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi na kuchangia kufikia dira ya maendeleo ya nchi.

Kwa hitimisho, ninatambua kuwa umoja na mshikamano wa wananchi wa Nzega Mjini ndiyo nguzo kuu ya safari yetu ya maendeleo. Kwa pamoja, tutaweza kufanikisha malengo yote tuliyojiwekea kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.