Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) leo Aprili 17, 2024 amekuwa geni rasmi kwenye ufunguzi wa Kongamano la Mwaka la Kujadili Mageuzi ya Sera za Mifumo ya Chakula, Uvuvi na Mitugo.

Kongamano hilo la siku 3 linaloendelea katika Ukumbi wa Mabeyo jijini Dodoma linawakutanisha wadau mbalimbali wa kilimo wa ndani na nje ya nchi likilenga kuwa Jukwaa la majadiliano kwa katika sekta hiyo ambapo wadau hao watatafakari miaka 10 ya mageuzi ya kisera chini, kujadili mitumo, changamoto na kupendekeza maeneo ya kuimarisha sera, mifumo ya chakula himilivu, jumuishi na endelevu.

Kongamano hilo limehuduhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo, Mhe. Mariam Ditopile Mzuzuri (Mb); na Mifugo and Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *